Monday, November 23, 2015

Picha: Vitanda vya wagonjwa vyatua Muhimbili kama ilivyoagizwa na Raisi Magufuli

Jana ilikuwa ni siku ya Ufunguzi wa Bunge la 11 ambalo lilifunguliwa na Muheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Joseph Pombe Magufuli ambapo alieleze mambo mengi ikiwemo matumizi mabaya ya pesa Serikalini! 

Ikiwa ni siku moja tu toka Muheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania afute sherehe ambayo ilipangwa kufanywa baada ya wabunge kuapishwa na pesa hizo kutumika kununua vitanda katika hospitali ya Muhimbili ambayo inakabiliwa na tatizo sugu la ukosefu wa vitanda. leo kazi imeanza imeanza na vidanda tayari vimefika Muhimbili.