Saturday, October 24, 2015

Barnaba aanzisha Label ya muziki ‘High Table Sound’, Tayari ameanza kusimamia wasanii

Muimbaji na mtunzi wa nyimbo, Barnaba, ameanzisha label ya kusimamia wasanii wa muziki iitwayo ‘High Table’ na tayari ameshawasaini wasanii wanne

Barnaba ameiambia E-News ya EATV kuwa wasanii ambao tayari wamesainishwa ni Ice Boy, Sia, Asia na Mula Fleva.

“Kuna Ice Boy yule anayerap alikuwa kwa Young Killer zamani, nimeshamchukua. Watu watashangaa kwanini Barnaba amechukua msanii wa kurap wakati yeye anaimba. Nimemchukua msanii wa kike anarap anaitwa Sia. Pia nina msanii wangu anawakilisha pande za Njombe, Mula Fleva. Nimemchukua na Asia yule anayeimba pia.”  Amesema Barnaba.