Saturday, October 17, 2015

Ommy Dimpoz ashoot video mbili ambazo zimefanyika Marekani na Afrika Kusini.

Baada ya ushindi wa tuzo ya Afrimma 2015, Ommy Dimpoz ali-tease nyimbo mbili tofauti Instagram akiashiria kuwa anakaribia kupakua wimbo mpya.
Katika post hizo mr PKP aliandika; “Vipi? Mko Tayari Baada ya Uchaguzi Tuachie MABODY?”, na nyingine “I can’t wait @nahreel on the beat”.

Lakini kuna uwezekano kionjo ulichokisikia kisiwe ni cha wimbo utakaotoka kwasababu bado yuko kwenye njia panda kuamua ni wimbo upi utangulie kutoka.

Staa huyo wa ‘Wanjera’ amesema tayari ameshoot video za nyimbo mbili, moja ikiwa imefanyika Marekani na nyingine Afrika Kusini.

Tayari nimeshashoot video mbili ambazo sijajua niachie ipi, kuna video nimeshoot Marekani na nyingine nimeshoot Afrika Kusini” alisema Ommy Dimpoz.

Lakini majibu yatapatikana baada ya uchaguzi, ambapo ndio amepanga kuachia wimbo na video mpya ambao amesema anaamini itakuwa ni hit.