Saturday, October 17, 2015

(Picha) Chris Brown akiwa na Mwanae "Royalty" Kwenye Cover ya Album yake Mpya.

Chris Brown ameendelea kuudhihirishia ulimwengu mapenzi ya dhati aliyonayo kwa mwanaye wa kike Royalty mwenye umri wa mwaka mmoja.
Baada ya kuamua album yake mpya kuipa jina la mwanaye huyo ‘Royalty’, sasa staa huyo wa R&B ametoa cover ya album hiyo yenye picha ya yeye akiwa amembeba mtoto wake anayeonekana amesinzia.

Toka Breezy afahamu kuwa ana mtoto na aliyewahi kuwa model Nia Guzman, amekuwa akionesha jinsi gani anajivunia kuwa baba na kwa kiasi gani mtoto huyo amemuongezea furaha kwenye maisha yake.

Album ya ‘Royalty’ imepangwa kutoka Nov.27.