Friday, November 6, 2015

Benpol aenda south kushoot video mpya

Pin It
Ben Pol ameongezeka kwenye orodha (inayozidi kuwa ndefu) ya wasanii wa Tanzania wenye mipango au walioishaenda Afrika Kusini kushoot video zao za muziki.


Ben Pol akiwa na Justin Campos na timu yake na Rossie M Afrika Kusini
King wa RnB ameamua kufunga safari kwenda Johannesburg kwaajili ya kushoot video ya wimbo wake mpya ‘Ningefanyaje’ aliowashirikisha Avril wa Kenya na msanii mpya Rossie M, ambayo amechagua kufanya na director Justin Campos wa Gorilla Films.
Kwanini kamchagua Justin Campos ?: “Nimekuja kushoot na Campos kwasababu Kiukweli haina ubishi Campos amefanya kazi nyingi nzuri sana na nyingi zina mafanikio. Na kuhusu kuuchagua ‘Ningefanyaje’ kuwa ndio wimbo wa kwanza kuufanyia video nje na director wa Nje: “Mimi naiamini Ningefanyaje sana na naamini kwamba kwa ubora wa video za Campos inaweza kwenda mbali zaidi” Ben Pol ameiambia Bongo5.
Ben amesema kuwa wanatarajia kushoot video hiyo Jumapili hii Nov.8.
Wasanii wengine ambao wameshoot video Afrika Kusini hivi karibuni ni pamoja na Harmonize ‘Aiyola’ ambayo imetoka leo, Vanessa Mdee ‘Never Ever’ (imetoka), Joh Makini ‘Don’t Bother’ ft. AKA na G-Nako ‘Original’(zinatoka hivi karibuni). Chege ft. Runtown ‘Sweety Sweet’ (Bado kutoka), Alikiba na Christian Bella ‘Nagharamia’ (Inatoka leo). Pia Ommy Dimpoz alisema ameshoot video mbili, moja Afrika Kusini na nyingine Marekani. Zingine zilizoisha toka ni pamoja na ‘Game’ ya Navy Kenzo, Jux ‘Looking For You’ na ‘Nana’ ya Diamond.
Kwa speed iliyopo sasa ya wasanii wa Bongo kuzidi kuwekeza kwenye video nzuri, kuna uwezekano mkubwa mwezi mmoja au miwili kuanzia sasa kutakuwa na video nyingi zaidi za wasanii wa Tanzania kwenye rotation pamoja na chati za TV kubwa kama MTV Base, Trace Tv, SoundCity pamoja na zingine.

Source Bongo5

Pin It

Add a comment

2 comments