Mshindi wa airtel trace music stars 2015 Africa Mayunga Nalimi anatarajiwa kuondoka nchini tarehe 16 mwezi huu (jumatatu) ili kurekodi nyimbo na Msanii maarufu wa marekani Akon.Ujumbe huo umetolewa na airtel wenyewe kupitia akaunti yao ya twitter pia Mayuunga aliwahi eleza kwamba kinacho mpeleka marekani ni kupata mentorship(mafunzo)..kurekodi nyimbo na kufanya video.
Mayunga alishinda kupitia airtel trace mkataba wa kurecord nyimbo kwenye studio za Universal music group kwa gharama ya $500,000 (1,000,000,000tzs)
Hivyo pia tutegemee mistari ya kingereza kwani wimbo huo hautaandikwa na mayunga bali akon mwenyewe.
Hata hivyo Mayunga july alishoot video yake south africa ya nice couple ambayyo ilipata nafasi ya kupigwa na Trace urban.


