Friday, November 6, 2015

Picha- Dk John pombe magufuli aapishwa kuwa rais wa watanzania



Dokta John Pombe Magufuli, Alhamis hii ameapishwa kuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hafla iliyohudhuriwa na wananchi pamoja na viongozi wa nchi mbalimbali barani Afrika.
ma35
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Pombe Magufuli akiapishwa Alhamis hii
Ikiwa ni siku iliyotangazwa na Rais aliyeondoka madarakani Jakaya Kikwete kuwa ya mapumziko, wananchi wengi walishuhudia kuapishwa kwa Magufuli kupitia runinga zao. Wengine walisikiliza matangazo kwenye redio.
ma36
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman akimuapisha Dokta John Magufuli kuwa Rais mpya wa Tanzania
Kitu kikubwa ambacho Tanzania itajivunia katika siku hiyo ni kuwa wananchi walionesha kuwa watulivu na kuendeleza ule utamaduni wetu uliozoeleka wa amani na upendo.
Awali kulikuwa na hofu kiasi iwapo siku hiyo ingemalizika bila vikwazo kutokana na namna uchaguzi ulivyomalizika hasa baada ya upinzani uliongozwa na vyama vinavyounda muungano wa Ukawa kudai kutoyakubali matokeo ya urais.
ma120
Tajiri namba moja wa Afrika, Aliko Dangote (katikati) ni mmoja wa wageni walioalikwa kwenye sherehe hizo. Kulia ni katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Magufuli na makamu wake, Samia Suluhu Hassan anayekuwa makamu wa rais wa kwanza mwanamke nchini, waliapishwa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam mbele ya jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman.
ma56
Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman akisaini hati ya kiapo ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan
Hotuba ya Dkt Magufuli ilikuwa fupi, ya unyenyekevu mkubwa na yenye ahadi za kuwatumikia wananchi wa Tanzania. Rais huyo aliupongeza upinzani kwa nguvu iliyokuwa nao katika uchaguzi wa mwaka huu na kuwataka kushirikiana katika kuiletea Tanzania maendeleo.
ma89
Rais wa awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisimama wima wakati wimbo wa Taifa ukipigwa na mizinga 21 ikipigwa
Alisema anawatambua kama walikuwa washindani wenzake na sio wapinzani wake. Alikiri kuwa anaingia ikulu akitambua kuwa ana deni kubwa kwa watanzania na ambalo atajituma kuhakikisha linalipwa.
“Tumepokea dhamana hii kwa unyeyekevu mkubwa, tunatambua kuwa tuna deni tuliloahidi na jukumu kubwa la kuwatumikia, nimejifunza mengi kutoka kwa wagombea wenzangu saba lakini tutambue kuwa nchi yetu ni kubwa kuliko vyama vyetu,” alisema.
ma105
Rais anayeondoka madarakani, Jakaya Kikwete akimpongeza Dokta Magufuli baada ya kuapishwa na kuchukua kiti chake. Wanaoshuhudia ni marais wa Rwanda, Uganda na Zimbabwe
Sherehe hizo zilihudhuriwa na marais wastaafu Mzee Ali hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Abeid Aman Karume. Viongozi wa waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Robert Mugabe (92) wa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
ma108
Wengine ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museven, Rais wa DRC, Joseph Kabila, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Rais wa Msumbiji,Filipe Nyusi.
Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Mohamed Gharib Bilal nao walihudhuria.
Hata hivyo mawaziri wakuu wa zamani Edward Lowassa aliyekamata nafasi ya pili kwenye uchaguzi huo na Frederick Sumaye hawakuhudhuria.
868231ee-a5b1-4003-8d42-9bc7b26beb3b
Mchungaji maarufu wa Nigeria, TB Joshua akiangalia matangazo kwenye TV akiwa na Edward Lowassa na mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe
Picha hiyo chini imevutia zaidi na kusambaa mtandaoni ikiwa kama meme.
297e1f95-8e22-4857-9db2-436b4848ca9c

PICHA KWA HISANI YA MICHUZI MATUKIO

source Bongo-5


Add a comment

0 comments