Wednesday, October 28, 2015

Breaking news : Matokeo yote ya Uchaguzi Zanzibar Yafutwa na Zec

Tume ya Uchaguzi Zanzibar imeufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar kutokana na kuwa na dosari nyingi ikiwemo uchaguzi kutokuwa huru na wa haki 

Mwenyekiti wa ZEC amewaambia waandishi wa habari mchana huu kuwa amechukua maamuzi hayo baada ya kujiridhisha kuwa uchaguzi ulighubikwa na dosari nyingi. 

"Mimi nikiwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, nimeridhika kuwa Uchaguzi huu umegubikwa na makosa makubwa.... 

"Kwa mamlaka niliyonayo natangaza rasmi kuufuta uchaguzi huu kwa kuwa haukuwa huru na wa haki, mtajuulishwa tarehe itakayofanyika uchaguzi mwengine hapo baadae, Ahsanteni kwa kunisikiliza"! - Jecha S. Jecha, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).