Baada ya kuacha na shamsa Ford msanii wa kizazi kipya ambaye pia ni mwanahiphop ameiambia website ya bongo five kwamba kiukweli hatembei na chagga empress(Chagga barbie
) kama ambavyo wengi wanadhani lakini ikitokea akawa nae atajisikia vizuri.
Maneno haya yametokea baada ya chagga empress kupost video akimwambia ney anampenda na nay alirepost na kuandika
“Love you too bby Mtag umpendae @chaggaempress @chaggaempress”.
Nay aliyesema haya baada ya kuulizwa
“Naomba tu watu wajue ni mwanamke ambaye ninampenda, nampenda the way alivyo ni mwanamke mzuri anavutia sio vinginevyo, labda ikija ikatokea akiwa mwanamke wangu itakuwa ni poa zaidi lakini for this time nampenda the way alivyo”
Nay aliendelea na kusema
“Mimi na Shamsa tulishaachana muda mrefu tumebaki washkaji ana bwana yake nafikiri watu wanaona kwenye page yake anampost, lakini mwisho wa siku nafasi ikishaachwa na mtu watu watajua wataona tu dalili, for this time sidhani kama natakiwa kuongea mengi sana nafikiri watu wataona, lakini watu wajue kwamba Chagga ni mwakamke ambaye nampenda namkubali amekuwa ni rafiki yangu wa karibu sana, ni mwanamke mzuri so haijafikia hatua ya kuwa na mahusiano ya kihivyo ila ikifikia watu wataona coz tuko karibu.”
NB:
Kama wengi wetu hatumfahamu chagga barbie yeye ni mwanadada wa kichagga ambaye aliwahi kutembea na msanii wa kenya prezzo baada ya mda waligombana sana matokeo yake chaga barbie alipost screen shot za prezzo akimponda Diamond na akimbembeleza chagga barbie,
Na ndugu zake prezo waliingili kati na kupost picha za chagga barbie akifanyiwa operesheni ya kuongeza makalio na kupunguza tumbo.




