Saturday, November 28, 2015

Ujumbe kutoka kwa Adam juma kwenda kwa madirector wachanga bongo

Director wa mda mrefu(mkongwe ) Adam juma ametoa ujumbe huu kupitia page yake ya instagram kwenda kwa upcoming directors hapa bongo.

“Kwa madirector wadogo na wakubwa, hakuna mafanikio yanakuja kirahisi rahisi, hakuna media itakayokuokoa katika ukame wa kazi utakapo wasili. Sifa hujenga kiburi akili hujenga ustaarabu, mafanikio yako yapo mkononi mwako- hata wakishot mbinguni isiwe sababu ya ww kuacha na kutoipenda kazi yako. Simama kwenye mstari na ujiamini, usishindane na upepo wa dunia hautashinda. Hakuna anayeweza akawa num 1 kila siku na ukilijua hili utalala vizuri bila stress. Kila kazi ya mikono yangu ni zawadi kwa atakaye ipenda na kuichukia, najiamini na naipenda kazi yangu. Ubunifu ndio utakao tuokoa katika ukame huu na sio budget, uongo, chuki na majigambo. Stay blessed all. AJ”